Wakaazi wa Nairobi ikiwemo Ikulu ya Rais kukosa maji

0

Baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Nairobi watakosa maji siku ya Jumatano na Alhamisi wiki hii.

Katika taarifa kampuni ya usambazaji maji kaunti ya Nairobi imesema kuwa hatua hio itatoa nafasi kwao kuboresha  mabomba ya  maji yaliyo katika maeneo ya Uthiru na Dagoreti.

Maeneo yatakayoathirika ni pamoja na yale yaliyo katika barabara za Naivasha, barabara ya Ngong, ile ya Langata na pia ile ya Waiyaki.

Miongoni mwa maeneo hayo ni Ikulu ya Rais, mitaa ya Riruta, Kawangware, Dagoretti Corner, Ngando, Kilimani, hifadhi ya maiti ya City, Hospitali ya kitaifa ya Kenyatta, ile ya Nairobi na hospitali ya Coptic.

Manaeo mengine ni pamoja na mitaa ya Lavington, Kileleshwa, Kibera, Langata, hospitali ya Forces memorial, shirika la Kemri na soko la Kenyatta.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here