Maafisa wa polisi wanamzuilia mwanafunzi wa kidato cha pili kutoka shule ya upili ya wavulana ya Friends School Namwela kaunti ya Bungoma kwa madai ya kuteketeza bweni la shule yao.
Idara ya upelelezi nchii DCI inasema mshukiwa mwenye umri wa miaka 18 alinaswa kwenye kamera za CCTV akimwagilia mafuta ya aina ya petrol bweni hilo kabla ya kuwasha moto.
Baada ya kuwaha moto, aliruka nje akitumia dirisha na moto ukateketeza bweni hilo bila chochote kutolewa ndani.
Mshukiwa atafikishwa mahakamani hii leo kujibu mashaka ya kusababisha uharibifu.