Rais Uhuru Kenyatta amemuomboleza aliyekuwa mbunge wa Juja Francis Waititu akimtaja kama kiongozi aliyechangia pakubwa katika maendeleo ya taifa la Kenya.
Akihutubu kwenye matanga ya mwendazake, Rais amesema Wakapee alivyofahamika na wengi aliwajali wakaazi wa eneo bunge lake na kuwatendea mema licha ya kuugua.
Rais Kenyatta amesema kuwa miradi iliyoachwa nyuma atahakikisha kuwa ataikamilisha ili kutimiza malengo yake.
Familia ya marehemu imemtaja mwendazake kama mtu aliyejitolea na kupenda kazi yake licha ya kuugua saratani kwa miaka mingi.
Mbunge huyo alifariki tarehe 22 mwezi uliopita wa februrai, akipokea matibabu katika hospitali ya MP Shah, kaunti ya Nairobi baada ya kuugua saratani ya ubongo.