Hatimaye chanjo million moja na elfu ishirini dhidi ya virusi vya corona imewasili humu nchini.
Ndege ya shirika la Qatar iliyobeba chanjo hiyo za Oxford/Astrazeneca ilitua nchini muda mfupi baada ya saa sita za usiku wa kuamkia leo na kupokelewa na maafisa wakuu serikalini wakiongozwa na waziri wa Afya Mutahi Kagwe na mwenzake wa Uchukuzi James Macharia
Chanjo hiyo inayolenga watu wasiozidi million moja katika awamu ya kwanza kwa sasa inahifadhiwa katika mabohari ya serikali mtaani Kitengela na itaanza kutolewa kwa wakenya muda wowote kuanzia hapo kesho.
Kagwe hata hivyo amekuwa mwepesi wa kutoa onyo kwa wakenya kuwa bado taifa halijashinda vita dhidi ya ufisadi na kuwataka wakenya kuendelea kuzingatia masharti ya kusalia salama.
Rais Kuwa wa Kwanza
Rais Uhuru Kenyatta, naibu wake William Ruto, aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga na waziri wa Afya Mutahi Kagwe wanatarajiwa kupokea chanjo dhidi ya corona Ijumaa hii.
Taarifa ambazo hazijadhibitishwa zinaashiria kuwa wanne hao watakuwa wa kwanza kupewa chanjo hiyo ambayo imewasili nchini usiku wa kuamkia leo.
Hatua hiyo inalenga kutoa hakikisho kwa wakenya kuwa chanjo hiyo ya Oxford/Astra Zeneca ni salama kwa matumizi na kuodnoa dukuduku miongoni mwa baadhi ya wakenya.