Watu 15 zaidi wafariki kutokana na corona

0

Kenya imeandikisha maambukizi mapya 88 ya ugonjwa wa corona kati ya sampuli 1,668 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii inafikisha 170,735 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini huku kiwango cha maambukizi kikiwa katika asilimia 5.3%.

Waliopona wamefikia 116,847 baada ya kupona kwa watu 71 zaidi huku wagonjwa 15 zaidi wakifariki na kufikisha idadi hiyo kuwa 3,172.

Kufikia sasa, waliopata chanjo dhidi ya ugonjwa huo ni 969,489 huku waliopata chanjo ya pili wakiwa 203.

Miongoni mwao ni wahudumu wa afya 160, maafisa wa usalama 17.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here