Polisi watibua mkutano wa UDA Meru

0

Polisi wametibua mkutano wa wagombea wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) huko Meru kwa madai ya kukosa kibali.

Kulingana na Polisi, wagombea hao waliandaa mkutano huo wa kisiasa ndani ya jumba la mikutano pasipo kufuata masharti ya usalama kuzuia msambao wa virusi vya corona.

Katibu wa UDA Veronica Maina amekashifu hatua hiyo akisema hawakuhitaji kibali kuandaa mkutano huo.

Kupitia taarifa, chama hicho kimewalaumu Polisi kutokana na na kile kimeaja kama kutumiwa kuwanyanyasa bure.

Kimemtaka Inspekta mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai kuchukua hatua na kukomesha matumizi ya Polisi kutumia nguvu kupita kiasi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here