Watu 132 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli 4,220 kupimwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 102,353.
Katika taarifa waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema watu 62 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 84,790.
Watu 3 zaidi wameaga na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 1,794.
Watu 360 wamelazwa katika hopitali mbalimbali wengine 1,292 wanashughulikiwa nyumbani.
Idadi ya watu walio hali mahututi ni 31.
Msambao katika kaunti ni kama ifutavyo Nairobi 96, Kiambu 8, Taita Taveta 6, Kisumu 6.