Mwanafuzi,17, afariki baada ya kupigwa Vihiga

0

Baba mmoja,52, ameshikwa huko Vihiga kwa madai ya kumpiga na kumuua mvulana mwenye umri wa miaka 17.

Mshukiwa John Shipiti anadaiwa kumshambulia kwa ngumi na mateke mwanafunzi huyo wa darasa la nane Agosti 7 mwaka jana na kumsababishia majereha ya mwili kwa kumshuku kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana wake mwenye umri wa miaka 13.

Kukamatwa kwake kumewadia baada ya kifo cha mvulana huyo mwanafunzi wa shule ya msingi ya Chemego katika hospitali ya Vihiga.

Marehemu alikuwa na majereha mabaya ya miguu, mashavu sawa na usoni na tukio hilo lilifichwa hadi alipokufa.

Mshukiwa huyo anazuiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa mauji baada ya upasuaji kufanyiwa mwili wa marehemu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here