Polisi huko Langa’ta, Nairobi wanamzuilia msichana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na tano kwa madai ya kumuua kwa kumdunga kisu mvulana mwenye umri wa miaka kumi na tisa anayesemekana kuwa mpenziwe.
Majirani wanasema wawili hao waligombana kabla ya msichana huyo mwanafunzi wa darasa la sita kuchukua kisu na kumdunga mwenzake mwanafunzi wa kidato cha pili kufuani.
Wameongeza kuwa wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu na kwamba tofauti ziliibuka baina yao kumhusu msichana mwingine.
Juhudi za kumuokoa mvulana huyo ziliambulia patupu kwani alifariki pindi alipofikishwa katika hospitali ya St. Mary’s.









