LSK wataka wabunge wanyimwe mishahara

0

Chama cha mawakili nchini (LSK) sasa kinataka wabunge kunyimwa mishahara na kunyanganywa walinzi kuanzia Agosti 12 iwapo rais Uhuru Kenyatta atakosa kulivunja bunge.

LSK kupitia rais wake Nelson Havi inasema bunge litakuwa linahudumu kinyume cha sheria baada ya Agosti 12 kufuatia hatua ya jaji mkuu David Maraga kumshauri rais kulivunja kwa kushindwa kupitisha sheria kuhusu usawa wa jinsia.

Havi anasema rais Kenyatta hana lingine ila kulivunja bunge na iwapo hilo litakosa kufanyika basi hawatakuwa na budi ila kuitisha maandamano ya kitaifa kumshinikiza kufuata sheria.

Wakati uo huo

Waangalizi wa uchaguzi ELOG wanamtaka rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge alivyoshauriwa na jaji mkuu David Maraga.

ELOG kupitia msimamizi wake wa mipango Mulle Musau ameambia bibliahusema.org/again/index.ph hiki kwamba Maraga alifanya anavyohitajika kikatiba kumshauri rais Kenyatta kuvunja bunge baada ya bunge kushindwa kupitisha sheria kuhusu usawa wa jinsia na rais hana lingine ila kuzingatia alivyoshauriwa.

Kuhusu uhalali wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kusimamia chaguzi ndogo katika maeneo bunge yote 290 iwapo bunge litavunjwa, ELOG wanasema hilo halina shaka yoyote kwani tume hiyo chini ya uongozi wake Wafula Chebukati  ina uwezo wa kusimamia chaguzi hizo na kuliwezesha taifa kuwa na wabunge wapya licha ya kuwa na makamishna wachache.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here