Makurutu watakaojiunga na KDF wafuzu

0

Rais Uhuru Kenyatta amewataka makurutu wanaofunzu ili kujiunga na kikosi cha wanajeshi nchini KDF kujituma zaidi na kufanya kazi kwa kujitolea.

Akiongoza hafla iliyofanyika katika shule ya mafunzo ya jeshi mjini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu baada ya kupokea mafunzo kwa muda wa miezi minane rais amesema kuwa makurutu hao watajiunga na vikosi mbalimbali vya usalama hivyo wafanye kazi kwa kujituma.

Rais pia amesema wanawakabidhiwa jukumu la kulinda nchi na mipaka yake na kukabiliana na visa vya kigadi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya hafla hiyo, wananchi hawajaruhusiwa kuhudhuria kutokana na masharti ya kuzuia msambao wa corona.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here