Serikali imeongeza muda kwa wanafunzi wa darasa la nane na wale wa kidato cha nne kujisajili kwa mitihani ya kitaifa ya KCPE na KCSE mtawalia, mwaka 2021.
Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema sughuli hiyo iliyoratibiwa kukamilika Jumamosi iliyopita sasa litakamilika tarehe kumi na nne mwezi huu.
Magoha anasema hatua hiyo itahakikisha kuwa hakuna mwanafunzi ambaye anawachwa nyuma na kuwataka walimu wakuu kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi aliyehitimu anasajailiwa.
Mitihani hiyo ya KCPE na KCSE mwaka 2021 itafanyika mwezi Machi hapo mwakani.
Kufikia Jumamosi, jumla ya wanafunzi 1,218,892 walikuwa wamesajiliwa kukalia mtihani wa KCPE katika vituo 28,248 kote nchini huku wanafunzi 824,392 wa kidato cha nne wakijisajili kukalia mtihani wa KCSE katika vituo 10,384.