Washukiwa wawili wa ugaidi wamekamatwa katika eneo la Merti kaunti ya Isiolo kwa kupatikana na silaha haramu usiku wa kuamkia leo.
Abdi Fatah Ibrahim na Yusuf Mohamed walipatikana na bunduki aina ya AK47, risasi 128 na magrunedi mawili.
Wawili hao walikuwa na magari mawili aina ya Toyota walipokutana na maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria kwenye barabara ya Duma-Yamicha.
Washukiwa hao wanahojiwa na maafisa wa kukabiliana na ugaidi huku uchunguzi zaidi ukiendelea.