Washukiwa saba wamekamatwa huku bunduki 35 zikishikwa kwenye oparesheni ya kiusalama inayoendelea katika eneo la Kapedo na Arabal.
Msemaji wa idara ya Polisi Charles Owino akiwahutubia waandishi wa habari amesema msamaha utatolewa kwa wenyeji watakaosalimisha silaha wanazomiliki kinyume cha sheria kwa hiari.
Amesema oparesheni hiyo itaendelea hadi waliohusika na mauji ya hivi punde ikiwemo afisa mmoja wa Polisi sawa na wizi wa mifugo watakaposhikwa na kuadhibiwa.