Katibu wa Baraza la Mawaziri, Mercy Wanjau, ametoa wito kwa serikali kuwashirikisha wananchi zaidi katika utekelezaji wa sera na mipango yake, akisema maoni na uzoefu wao ni muhimu katika kuboresha huduma kwa umma.
Wanjau amesema wakati umefika kwa serikali kuwasikiliza wananchi, kupokea maoni yao kikamilifu na kufanya marekebisho yanayofaa” kulingana na mahitaji na uzoefu wao.
Amesema Kenya ina fursa nyingi, hasa kwa vijana, akieleza kuwa ushirikiano kati ya serikali na wananchi ni muhimu katika kutumia fursa hizo.
“Kenya ina fursa nyingi kwa vijana leo. Kuna fursa nyingi zenye matumaini,” amesema Wanjau.
Wanjau pia amesema baadhi ya maamuzi ya serikali huchukua muda kutekelezwa kwa sababu mchakato huo huhusisha maandalizi, uratibu, tathmini ya rasilimali na kuzingatia changamoto zinazoweza kujitokeza.
“Wakati Baraza la Mawaziri linapoketi, maandalizi mengi, uratibu na mijadala muhimu huwa tayari imefanyika. Baraza hukutana kuzingatia chaguo zilizopo, hatari zinazoweza kujitokeza na rasilimali zinazohitajika kwa utekelezaji.” Wanjau ameongeza.









