Wakili Paul Gicheru atafikishwa mbele ya mahakama ya uhalifu wa kivita ICC mjini the Hague, Uholanzi hapo kesho (Ijumaa) ambapo anatuhumiwa kuwahonga mashahidi kwenye kesi za Kenya katika mahakama hiyo.
Gicheru aliyejisalimisha katika mahakama hiyo baada ya waranti ya kukamatwa kutolewa dhidi yake anatazamiwa kufika mbele ya jaji Reine Adelaide.
Atakapofika mbele ya mahakama hiyo, mtuhumiwa atahamishwa mashtaka dhidi yake, kisha afahamishwe haki zake chini ya mkataba wa Roma kabla ya kuelezewa hatua zitakazofuatwa kuhusu kudhibitishwa kwa mashtaka yanayomuandama.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Fatou Bensouda unadai kuwa Gicheru aliwahonga mashahidi wa mahakama hiyo na hivyo kutatiza mchakato wa kupatikana kwa haki.
Wakili Gicheru atashtakiwa pamoja na mwenzake Philip Bett ambaye yuko mafichoni tangia mwaka 2015 wakati kibali cha kukamatwa kwao kilitolewa.









