Kenya imeandikisha idadi kubwa ya maambukizi ya corona baada ya watu 1,494 kupatikana na ugonjwa huo kati ya sampuli 8,839 zilizopimwa katika muda saa Ishirini na nne zilizopita.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii inafikisha 58,587 idadi ya jumla ya visa vya ugonjwa huo nchini.
Watu wengine 586 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 38,381.
Wagonjwa wengine 12 wamefariki kutokana na makali ya ugonjwa huo kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,051.
Kwa sasa kuna wagonjwa 1,313 ambao wamelazwa katika hospitali mbalimali, 5,005 wanashughulikiwa nyumbani, 57 wamelazwa katika vyumba vya wagongwa mahututi, 25 kati yao wakisaidiwa na mashine kupumua.
Kaunti ya Nairobi inaongoza na visa 414, ikifuatiwa na Nakuru na visa 188, Mombasa 173 na Kiambu 150.