Makachero kutoka idara ya upelelezi DCI wamewashika washukiwa wawili kuhusiana na mauaji ya jamaa mmoja ambaye mwili wake ulipatikana kando ya barabara ya Mai Mahiu, Narok.
Wawili hao David Nago, (29) na Saitoti Sego (20) walikamatwa katika eneo la Ongata Rongai kaunti ya Kajiado kufuatia uchunguzi.
Washukiwa hao wamekamatwa baada ya Polisi kufahamishwa kuwahusu na walipofanya msako katika makaazi yao walipata nguo zilizo na damu na zitakuwa zinafanyiwa uchunguzi wa DNA.
Mwili wa marehemu unaarifiwa kuwa wa jamaa yao mwenye umri wa miaka 30.