Wakili Ken Nyaundi akataa uteuzi wa uenyekiti wa Azimio

0

 

Mrengo wa Azimio la Umoja umepata pigo baada ya mwanasheria tajika, Wakili Ken Nyaudi, kukataa uteuzi wake wa kuwa mwenyekiti wa muungano huo.

Baraza Kuu la Azimio, linaloongozwa na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, lilikuwa limemteua Nyaudi kuchukua nafasi ya Waziri wa Ushirika na Biashara Ndogo Ndogo, Wycliffe Oparanya.

Hata hivyo,Wakili Nyaudi amesema kuwa baada ya kufanya mashauriano ya kina, ameamua kukataa uteuzi huo bila kueleza kwa kina sababu za uamuzi wake.

Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya Baraza Kuu la Azimio kutangaza mabadiliko makubwa ya uongozi kufuatia mkutano ulioongozwa na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Katika mabadiliko hayo, kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, aliteuliwa na kuidhinishwa kuwa kiongozi wa mrengo wa Azimio la Umoja, akichukua nafasi ya hayati Raila Amollo Odinga.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema uteuzi wa Kalonzo Musyoka unamweka katika nafasi nzuri ya kupeperusha bendera ya upinzani katika uchaguzi mkuu ujao.

Aidha, Mbunge wa Suba Kaskazini, Caroli Omondi, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Azimio la Umoja, akichukua nafasi ya Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Taifa, Junet Mohammed.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here