Wakenya ‘wakerwa’ na safari ya wabunge Dubai

0

Baadhi ya wakenya mtandaoni wameelezea kukerwa na hatua ya wabunge kumi na sita kuelekea katika milki za Kiarabu kupata mafunzo kuhusu matumizi ya pesa za umma.

Wakirejea picha zilizotiwa mtandaoni na mbunge wa Nyali Mohammed Ali ambaye ni mmoja wa wabunge wanaoudhuria mafunzo hayo jijini Dubai, baadhi ya wakenya hao mtandaoni wanahisi kuwa safari hiyo inawadia wakati usiofaa kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha na pia maambukizi ya virusi vya corona.

Wabunge hao wa kamati mbalimbali za fedha wakiongozwa na kiongozi wa walio wachache John Mbadi wanasema mafunzo hayo yanalenga kuwasaidia katika uchunguzi wao kuhusu matumizi ya pesa za mlipa ushuru nchini.

Kinaya ni kwamba, kila mbunge anayehudhuria kongamano hilo anaripotiwa kupata marupurupu ya shilingi elfu mia moja na arobaine na tatu kila siku, kumaanisha kuwa mlipa ushuru atatoa zaidi ya shilingi million ishirini kuwapa marupurupu wabunge hao ambao walielekea Dubai Alhamisi wiki iliyopita.

Hii ina maana kuwa kila mbunge aliye Dubai anatazamiwa kupata takribani shilingi million moja nukta mbili nane.

Kando na hayo, ripoti zinaashiria kuwa mlipa ushuru atatoa shilingi million mbili kugharamia usafiri wao kwani kwa mujibu wa shirika la ndege la Kenya Airways, kuenda Dubai na kurudi ni shilingi elfu mia moja arobaine na tatu kwa mtu mmoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here