Afisa wa polisi amuua mwenzake kabla ya kujiua Nyamira

0

Afisa wa polisi amewapiga risasi wenzake wawili na kusababisha kifo cha mmoja wao kabla yake kujitoa uhai pia katika kituo cha polisi cha Nyamira.

Mmoja wa maafisa waliopigwa risasi alifariki akipokea matibabu hospitalini huku mwenzake akiendelea kutibiwa katika hospitali ya Nyamira Level 5.

Afisa aliyewamiminia risasi pia amefariki baada ya kujipiga risasi ya kichwa.

Chanzo cha mkasa huo uliotokea jana usiku hakijabainika huku polisi wakianzisha uchunguzi.

Kisa hiki kinajiri wiki moja tu baada ya afisa mwingine wa kitengo cha GSU kumuua mwenzake kabla ya kujipiga risasi na kufariki papo hapo katika kambi ya polisi cha Chepchoina kaunti ya Trans Nzoia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here