Wahudumu wa afya katika kaunti ya Mombasa hatimaye wamesitisha mgomo wao uliodumu kwa muda wa miezi mitatu.
Wahudumu hao wakiwemo Wauguzi na Matatibu wameafikia makubaliano ya kurejea kazini na serikali ya gavana Hassan Joho.
Katibu wa muungano wa Wauguzi KNUN tawi la Mombasa Peter Maroko anasema walikuwa na malalamishi kumi na moja ikiwemo mishahara na kutopandishwa vyeo.
Tusalie na hayo ya afya ambapo
Viongozi wa kidini katika kaunti ya Taita Taveta wamekashifu kufurushwa kwa wahudumu wa afya kutoka kwa nyumba za serikali.
Wahudumu zaidi ya mia tatu walifurushwa kutoka kwa nyumba hizo baada kususia kurejea kazini wakati wa mgomo viongozi hao sasa wanaitaka serikali ya Granton Samboja kutoa suluhu la kudumu kwa wahudumu hao wa afya.









