Tuju awaita MCAs wa Uasin Gishu kwa mkutano Nairobi

0

Katibu mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju ameitisha mkutano na madiwani 17 wa chama hicho katika kaunti hiyo ya Uasin Gishu Ijumaa.

Bunge hilo la Uasin Gishu linatazamiwa kupiga kura ya kuamua hatma ya mswada huo wiki ijayo.

Mkutano huo unaandaliwa katika makao makuu ya chama hicho jijini Nairobi.

Mabunge 11 tayari yamepitisha mswada huo huku bunge la kaunti ya Baringo likiwa na pekee lililokataa kuidhinisha mswada huo kufikia sasa.

Mabunge yaliyopitisha mswada huo ni pamoja na Kisii, Vihiga, Laikipia, Nairobi, Kisii, Kajiado, Trans Nzoia, Pokot Magharibi, Busia, Homa Bay, Kisumu na Siaya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here