Wahudumu wa afya Kisumu mgomoni tena (Audio)

0

Baadhi ya wahudumu wa afya katika kaunti ya Kisumu wameanza  mgomo wao hii leo kulalamikia kutolipwa mishahara yao ya hadi miezi sita.

Wahudumu hao walioajiriwa Oktoba mwaka uliopita wanalalama kuwa serikali ya Gavana Profesa Peter Anyang Nyongo imewaandikia barua inayosema wahudumu hao hawako kwenye orodha ya wafanyikazi wanaofaa kupokea mishahara

Migomo ya wahudumu wa afya imekuwa ikishuhudiwa katika kaunti mbalimbali  nchini kulalamikia malipo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here