Kamati ya bunge la kitaifa kuhusu haki na masuala ya kisheria imeidhinisha uteuzi wa Anne Nderitu kuwa msajili wa vyama vya kisiasa.
Kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Kangema Clement Muturi Kigano pia imeidhinisha uteuzi wa Florence Tabu na Ali Abdullahi kuwa wasaidizi wa Nderitu lakini wakatupilia mbali uteuzi wa Wilson Mohochi aliyependekezwa na Rais Uhuru Kenyatta kuwa msaidizi pia.
Nderitu ambaye amekuwa akishikilia wadhfa huo kama kaimu kuanzia mwaka 2018 sasa anasubiri idhini ya bunge kabla ya kuteuliwa rasmi na Rais ili aendelee na majukumu yake.
Bunge litajadili ripoti ya kamati hiyo na kuamua hatma ya wanne hao.