Idadi ya maafa yanayotokana na ugonjwa wa corona yanaelekea kupindukia elfu mbili baada ya wagonjwa 17 zaidi kufariki katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi hiyo kuwa 1,954.
Na kwa siku ya tatu mtawalio, maambukizi mapya zaidi ya elfu moja yamedhibitishwa nchini huku visa 1,225 vikiripotiwa kati ya sampuli 7,308 zilizopimwa na kufikisha idadi visa hivyo nchini kuwa 117,535.
Wizara ya afya imedhibitisha kupona kwa watu 142 zaidi na kufika idadi ya waliopona kuwa 89,203.
Wagonjwa waliolazwa katika chumba cha watu mahutui ICU ni 114, wagonjwa 793 wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini huku wengine 2,250 wakishughulikiwa nyumbani.