Wenye matatu nchini wametishia kuongeza nauli kufuatia kupanda kwa bei za mafuta.
Kupitia kwa mwenyekiti wao Simon Kimutai, muungano wa wenye matatu (MOA) umesema utapandisha nauli kwa sababu serikali imepandisha mafuta kwa shilingi 20.
Kimutai amesema masharti yaliyowekwa na wizara ya afya ili kuzuia msambao wa virusi vya corona ikiwemo kubeba abiria nusu yamefanya hali kuwa ngumu zaidi.
Na sasa wanaitaka serikali kuwaruhusu kubeba abiria kama kawaida kabla ya kuingia kwa corona kwa sababu ndege zimeruhusiwa kubeba abiria wakiwa wamejaa.