Wabunge wametishia kutatiza kusomwa kwa bajeti Alhamisi baada ya Waziri wa fedha Ukur Yattani kuwanyima pesa za ustawishaji maeneo bunge CDF kabla ya kukamilika kwa mwaka huu wa kifedha.
Mbunge wa Aldai Cornelly Serem anasema kutowasilishwa kwa CDF kumetatiza ufadhili wa masomo ya watoto haswaa kutoka familia maskini sawa na kulemaza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande mwingine, Wakenya wanamtarajia waziri Yattani kuwapa afueni atakaposoma bajeti ya mwaka 2021/2022 inayogharimu Shilingi Trilioni tatu nukta sita.
Kibarua ni kwa waziri Yattani kuweka kwenye mizani kurejesha uchumi baada ya janga la corona na kutimiza ajenda nne za rais Uhuru Kenyatta.









