Aliyekuwa Jaji Mkuu Dkt. Willy Mutunga amekuwa wa hivi punde kujitosa kwenye malumbano yanayoendelea kuhusu kuapishwa kwa majaji sita ambao rais Uhuru Kenyatta alikataa kuwateua rasmi.
Dkt. Mutunga ambaye ni Jaji Mkuu wa kwanza chini ya katiba ya mwaka 2010 amemshauri rais Kenyatta kuwaapisha majaji hao kwa sababu hilo ndilo jambo sahihi kufanya kwa sasa.
Kwenye barua yenye maneno makali, Mutunga amesema iwapo rais alikuwa na maswali kuwahusu majaji hao, basi angawasilisha lalama zake kwa tume ya huduma za mahakama JSC kwa wakati unaofaa na wala sio sasa hivi.
Amemtaka rais kuwateua majaji hao mara moja akihoji kwamba kuchelewa kufanya hivyo ni kutumia visivyo mamlaka yake.









