Wabunge wanne wa mrengo wa Tangatanga wameshikwa huku uchaguzi mdogo wa Kabuchai ukiendelea.
Wanne hao Didmus Barasa wa Kimilili, mwenzake wa Belgut Nelson Koech, Wilson Kogo wa Chesumei na Seneta wa Nandi Samson Cherargei wamekamatwa wakati ambapo kunaripotiwa madai ya visa vya wapiga kura kuhongwa huku upigaji kura unaendelea.
Watatu hao wamepelekwa katika kituo cha Polisi cha Bungoma.
Awali, kiongozi wa chama cha FORD Kenya Moses Wetangula alidai kuwepo kwa visa vya wapiga kura kuhongwa na baadhi ya wabunge wanaomuunga mkono muwanaji wa chama cha United Democratic Alliance (UDA).
Katika wadi ya Kiamokama kaunti ya Kisii, Polisi wamewashika washukiwa wanne kwa madai ya kuwahonga wapiga kura.
Mwanasiasa Don Bosco Gichana vile vile alikamatwa na maafisa wa usalama kwa tuhuma zizo hizo za kuwahonga wapiga kura.









