Polisi wanamtafuta aliyekuwa waziri wa Michezo Rashid Echesa baada yake kunaswa kwenye video akimchapa kofi afisa wa tume ya uchaguzi IEBC katika kituo cha kupigia kura cha Bulonga eneo bunge la Matungu.
Mwenyekiti wa tume ya IEBC Wafula Chebukati amekashifu tukio hilo na kuwataka maafisa wa usalama kuhakikisha kuwa inawazuia watu ambao hawana vibali kuingia katika vituo vya kupigia kura.
Katika wadi ya London, kaunti ya Nakuru; upigaji kura umetatizwa baada ya vuta nikuvute baina ya maajenti wa chama cha UDA na maafisa wa Polisi.
Aidha mbunge wa Langata Nixon Korir amelalamikia kupigwa na wahuni huku Polisi wakitizama.









