Wabunge 41 wa Mlima Kenya wadai Raila hauziki huko kwao na BBI sio maarufu

0

Wabunge wapatao 41 kutoka eneo la Mlima Kenya wamemuandikia rais Uhuru Kenyatta barua wakisema ripoti BBI sio maarufu katika eneo hilo la kati.

Katika barua hiyo, wabunge hao aidha wamesema imekuwa vigumu kumuuza Raila Odinga katika eneo hilo kisiasa licha ya ushirikiano uliopo kupitia handisheki.

Wabunge hao wamemlaumu rais Kenyatta kutokana na kile wametaja kama kuwasaliti na hivyo kuwafungia nje ya mkutano wa Jumamosi huko Sagana kaunti ya Nyeri.

Sehemu ya barua hiyo inaeleza kuwa rais amekuwa akiwaambia kuwa Raila anafaa kustaafu kutoka kwa sasa jambo ambalo amefanya kuanzia mwaka 2013 hadi 2018 na kinachowashangaza ni namna amewagauka na sasa anawataka kumuuza kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Mkutano huo wa Sagana unatazamiwa kujadili mwelekeo wao kisiasa utakaochukuliwa na eneo la hilo.

Mbunge wa Kieni Kanini Kega anasema kuwa mkutano huo utajadili kilimo cha kahawa, majani chai na mbinu za kuinua vijana kifedha.

Kega amesema kuwa viongozi wa mlima Kenya wanaaunga mkono ripoti ya BBI kwa sababu italeta umoja haswa wakati wa uchaguzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here