Mashirika yataka misaada ikubaliwe Kapedo

0

Mashirika yasiyo ya serikali katika kaunti ya Baringo yanaitaka serikali kuruhusu misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula na vifaa vya matibabu kwa familia zilizoathirika kwenye oparesheni ya kiusalama inayoendelea Kapedo.

Mashirika hayo vile vile yanatoa wito kwa asasi za usalama kuviruhusu vyombo vya habari kuingia katika eneo hilo na kuripoti kuhusu oparesheni hiyo pasipo kuingiliwa.

Yakiongozwa na mwenyekiti wa mashirika hayo Baringo Philip Tomno, watetezi hao wa haki za kibinadamu wameelezea wasiwasi wao kuhusu namna oparesheni hiyo inavyoendelezwa huku umma ukikosa ufahamu kuhusu yanayojiri.

Kwa upande mwingine, mwanaharakati Evans Kibet amelalama kwamba makundi tengwa kama vile walemavu, wazee, akina mama na watoto wamejipata pabaya wakati wa oparesheni hiyo bila msaada wa kiutu.

Kufikia sasa watu kumi wamepoteza maisha wakiwemo maafisa wa Polisi kufuatia visa vya utovu wa usalama katika eneo hilo hali iliyochangia kuanzishwa kwa oparesheni hiyo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here