Vikosi vya KDF vyaelekea mjini DRC kuleta amani

0

Wanajeshi wa Kenya wameelekea nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kusaidia katika kupambana na magaidi.

Vikosi hivyo inatarajiwa kutekeleza jukumu muhimu la kuleta amani nchini DRC na kuwalinda wafanyikazi wa shirika la Umoja wa Mataifa (UN).

Wanajeshi hao vile vile wanatazamiwa kupambana na makundi yaliyojihami ambayo yamekuwa yakiwahangaisha raia wa taifa hilo.

Kenya ilikubali kuwatuma wanajeshi wake kufuatia makubaliano baina ya rais Uhuru Kenyatta aliyezuru Kinshasa na mwenyeji wake Felix Tshisekedi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here