Vikao vya kesi ya mauji dhidi ya Sharon Otieno vyahairishwa

0

Awamu ya kwanza ya vikao vya kusikilizwa kwa kesi ya mauji dhidi ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno imekamilika Alhamisi.

Jaji wa Mahakama ya Milimani anayesikiliza kesi hiyo Cecilia Githua ameratibu awamu ya pili kuanza Octoba 4 hadi Octoba 7 huku awamu ya tatu na ya mwisho ikiratibiwa kuanza Disemba 6 hadi Disemba 9.

Kwenye vikao vya Alhamisi, afisa wa Polisi wa Homa Bay Willy Okoti amesimulia alivyompokea mwanahabari aliyedai kuwa alikuwa ametekwa nyara pamoja na Sharon.

Okoti ameiambia mahakama kwamba mwanahabari huyo alikuwa anatokwa na damu mikononi na miguuni baada ya kujirusha kutoka kwa gari lililokuwa linaendeshwa kwa mwendo wa kasi.

Wakili wa washtakiwa Tom Ojienda aliyepewa nafasi ya kumuuliza maswali afisa huyo ametaka kujua ni vipi sehemu ya nyumba ya afisa huyo ilikuwa inatumika kama kituo.

Mahakama imeambiwa kwamba uchunguzi wa DNA unaonesha kwamba mimba ya wiki Ishirini na nane aliyokuwa amebeba Sharon ilikuwa ya gavana wa Migori Okoth Obado ambaye ameshtakiwa kwa mauaji hayo.

Mahakama hiyo aidha imefahamishwa kwamba huenda Sharon alidulumiwa kimapenzi kabla ya kuuawa huku mwili wake ukipatikana na majeraha zaidi ya saba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here