Awamu ya pili ya kampeini ya Polio kuanza Jumamosi hii

0

Awamu ya pili ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio itafanyika kuanza Jumamosi hii ya Julai 17 na kuendelea hadi Jumatano ijayo Julai 21.

Kaunti 13 ikiwemo; Garissa, Isiolo, Kajiado, Kiambu, Kilifi, Kitui, Lamu, Machakos, Mandera, Mombasa, Nairobi, Tana River & Wajir zinalengwa kwenye kampeini hiyo.

Wizara ya afya inawalenga watoto milioni 3.4 kwenye awamu hiyo ya pili.

Wahudumu wa afya watatembea kutoka nyumba hadi nyumba kutoa chanjo hiyo kwa watoto ili kuzingatia masharti ya kuzuia msambao wa corona.

Takriban watoto milioni 2.6 walipewa chanjo hiyo kwenye awamu ya kwanza iliyofanyika kati ya Mei 22 hadi Mei 26 mwaka huu wa 2021.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here