UNHRC watoa mwongozo wa kufungwa kwa kambi za Dadaab na Kakuma

0

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) limetoa mwongozo wa kufunga kambi za Dadaab na Kakuma kama lilivyoelekezwa na serikali ya Kenya.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kuwarejesha wakimbizi hao makwao kwa njia ya kiutu na kuzingatia masharti yaliyopo kuzuia msambao wa virusi vya corona, kuwa na mbinu mbadala kuwawezesha wakimbizi hao kusalia nchini haswaa wale kutoka Afrika Mashariki.

Fathiaa Abdalla mwakilishi wa shirika hilo nchini Kenya vile vile anaitaka serikali kuwapa vitambulisho vya kitaifa wakimbizi wapatao 11,000 ambao awali walitambuliwa na kusajiliwa baada ya kukaguliwa.

Shirika hilo vile vile linaiomba Kenya kuwawezesha wakimbizi ambao watahisi kwamba sio salama kurejea makwao kuhamishwa hadi katika mataifa mengine ambayo ni salama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here