Naibu rais William Ruto amemuomboleza mwanasiasa Ahmed Ibrahim aliyefahamika na wengi kama Johnny.
Ruto amemtaja Johnny kama kiongozi aliyeheshimiwa na hakuwa mbinafsi.
Johnny aliyewania kiti cha ubunge cha Kamukunji kwa tiketi ya chama cha ODM amefariki siku chache baada ya kupewa chanjo ya Sputnik.
Kiini haswaa cha kifo chake hakijabanika ila wendani wake wanasema amekuwa akikumbwa na matatizo ya figo.
Waliomfahamu wamemtaja kama mnyenyekevu na aliyekuwa mtu wa kutangamana na watu kwa urahisi.