UDA watamba London, ODM wakiwika Kisii

0

Anthony Nzuki wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinachohusishwa na naibu rais William Ruto ndiye diwani mpya wa wadi ya London kaunti ya Nakuru baada ya kutangazwa mshindi kwenye uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa.

Tume ya uchaguzi na mipaka IEBC imemtangaza Nzuki mshindi baada ya kupata kura 1,707 dhidi ya kura 1,385 alizopata mpinzani wake wa karibu Francis Njoroge wa chama tawala cha Jubilee.

Katika wadi ya Hell’sgate kaunti ya Nakuru, chama cha Jubilee kimehifadhi kiti hicho huku Virginia Wamaitha Gichanga akitangazwa mshindi kwa kupata kura 3,955 na kumshinda Jonathan Warothe wa UDA aliyepata kura 2,742.

Chama cha Jubilee vile vile kimehifadhi kiti cha wadi ya Huruma kaunti ya Uasin Gishu baada ya Lucy Ng’endo kutangazwa mshindi kwa kupata kura 2,498.

Katika wadi ya Kiamokama kaunti ya Kisii, Malack Mainya Matara wa chama cha ODM ameshinda uchaguzi huo kwa kupata kura 1,907 na kumshinda Nyakundi Daniel Ondabu wa chama cha Party of Economic Democracy (PED) aliyepata kura 1,257 na kufuatiwa na Stephen Magutu wa chama cha The New Democrats (TND). Moses Nyandusi Nyakeremba wa UDA alimaliza wa sita na kura 491.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here