Chama cha FORD Kenya kinachoongozwa na Moses Wetangula kimehifadhi kiti cha ubunge cha Kabuchai baada ya muwaniaji wake Majimbo Kalasinga kushinda uchaguzi mdogo ulioandaliwa Alhamisi.
Kalasinga ambaye amekuwa akiwania kiti hicho mara tatu bila kufaulu ametangazwa mshindi na tume ya uchaguzi IEBC baada ya kupata kura 19,274 dhidi ya mpinzani wake Evans Kaikai wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinachohusishwa na naibu rais William Ruto aliyeibuka wa pili kwa kupata kura 6,445.
FORD K wamehifadhi kiti hicho kilichosalia wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa eneo bunge hilo James Mukwe Lusweti.