Tume ya huduma za walimu nchini (TSC) imeelezea matumaini yake kwamba itatia saini makubaliano ya maelewano na walimu baada ya mkutano wa Jumannejh.
TSC imekuwa kwenye mkutano wa pili na miungano ya walimu ya KNUT na KUPPET kuanzia asubuhi kushauriana kuhusu mkataba wa maelewano yaani CBA wa 2021-2025.
Mkutano wa juma lililopita ulitibuka baada ya kukosa kuelewana kuhusu nyongeza ya mishahara kwa walimu.
Katibu mkuu wa KNUT Collins Oyuu alisema walikataa ofa waliyopewa na mwajiri wao kwa msingi kuwa haikuwa na manufaa yeyote kwa walimu kando na likizo wakati wa kujifungua.