Tofauti zaibuka bungeni kuhusu mswada wa BBI

0

Kivumbi kimeshuhudiwa bungeni Alhamisi huku mjadala mkali ukishuhudiwa kuhusu mswada wa marekebisho ya katiba BBI.

Bunge la kitaifa liliongeza muda wa vikao vyake vya asubuhi hadi alasiri huku muda wa kuchangia ukipunguzwa hadi dakika saba ili kuwapa wabunge wengi nafasi ya kuchangia mswada huo.

Wabunge wanaounga mkono mswada huo wakiongozwa na Mishi Mboko walitetea mswada wenyewe wakihoji kwamba utawaletea Wakenya manufaa mengine ikiwemo fedha mashinani.

Hata hivyo aliyekuwa kiongozi wa wengi Aden Duale amewaongoza wenzake kupinga mswada huo kwa misingi kwamba utarudisha nyuma hatua ambazo taifa hili limepiga katika maswala ya uongozi.

Wabunge wanatofautiana kuhusu mswada huo licha ya uamuzi uliotolewa na spika Justine Muturi kwamba bunge hilo halina mamlaka ya kubadili mswada huo.

Malumbano haya yanashuhudiwa huku rais Uhuru Kenyatta na kinara wa chama cha ODM wakiwataka wabunge kuwaruhusu Wakenya kufanya maamuzi ya mwisho kuhusu mswada huo kupitia kwa kura ya maamuzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here