Otiende Amollo ajitetea baada ya kufurushwa

0

Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo ametaja kama uongo madai kwamba alituma ujumbe wa kumtishia kiongozi wa chama chake cha ODM Raila Odinga.

Mwenyekiti wa chama hicho John Mbadi amenukuliwa akidai kwamba Amollo aling’olewa kwa mafasi ya naibu mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu sheria (JLAC) kwa tuhuma kwamba alimtumia Odinga ujumbe wa kutishia kujiuzulu kwenye kamati hiyo.

Hata hivyo mbunge huyo wa Rarieda katika kujitetea kwake amesema hiyo ni porojo inayoenezwa na watu wanaotaka alaumiwe bure.

Ameongeza kwamba kufurushwa kwake kwenye kamati hiyo hakuhusiani kwa vyovyote na mtazamo wake kuhusu mswada wa marekebisho ya katiba BBI.

Nafasi ya Otiende Amollo kwenye kamati hiyo imetwaliwa na mwenzake wa Ruaraka TJ Kajwang’.

Chama cha ODM vile vile kimekanusha kuwepo kwa njama ya kumuondoa seneta wa Siaya James Orengo kwenye wadhifa wa kiongozi wa walio wachache kwenye bunge la Senate.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here