Tahadhari yatolewa kwa Wakenya, maambukizi ya corona yakizidi

0

Hospitali zimetakiwa kuongeza idadi ya vyumba vya kuwashughulikia watu mahututi (ICU) huku Kenya ikiripoti maambukizi mapya 1,279 ya corona kati ya sampuli 7,450 zilizopima katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kutokana na kuongezeka kwa visa vya ugonjwa huo katika wimbi hili la tatu, kaunti mbalimbali sasa zitaanza kuwashughulikia wagonjwa wake kwa sababu hospitali za Nairobi zimejaa.

Waziri Kagwe vile vile amesema familia zijiandae kuwashughulikia wagonjwa wa corona nyumbani kutokana na kujaa kwa hospitali nyingi huku akiwataka maafisa wa Polisi kuhakikisha kuwa umma umezingatia kikamilifu masharti ya kuzuia msambao wa virusi hivyo.

Idadi ya watu waliopona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita ni 280 na kufikisha idadi hiyo kuwa 89,061 huku maafa yakifikia 1,937 baada ya kufariki kwa wagonjwa 12 zaidi.

Hayo yaijiri

Watu 20,000 wamepata chanjo ya corona tangu zoezi hilo lilipoanza juma lililopita.

Akitoa hakikisho kwa Wakenya kwamba chanjo hiyo ni salama, waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema wengi waliochanjwa ni wahudumu wa afya huku walio na umri wa zaidi ya miaka 60 wakipewa kipau mbele.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here