Jennifer Wambua: Kesi yakosa kuendelea

0

Hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Francis Andayi amesikitikia kifo cha Jennifer Wambua aliyekuwa shahidi kwenye kesi ya ulaghai inayogharimu Sh122.3M.

Marehemu alikuwa ametoa ushahidi kwenye kesi hiyo ambapo mbunge wa Lugari Ayub Savula na aliyekuwa katibu mkuu Sammy Itemere pamoja na watu wengine 28 walishtakiwa kwa tuhuma za kushirikiana kuibia serikali Sh122.3M.

Andayi amehairisha kesi hiyo hadi kesho Alhamisi kuratibu tarehe mpya ya kuisikiliza kwani alifahamishwa leo kuhusu mauaji ya Wambua.

Wambua, naibu mkurugenzi wa mawasiliano katika tume ya ardhi nchini NLC alipatikana ameua Jumatatu na mwili wake kutupwa msituni Ngong baada ya kutoweka Jumamosi iliyopita.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here