Idara ya utabiri wa hali ya anga imetoa tahadhari ya kutokea kwa mafuriko katika kaunti tatu zinazopakana na taifa jirani la Ethopia.
Mafuriko hayo yanatazamiwa kushuhuhudiwa katika maeneo ya Marsabit, Mandera na Wajir kuanzia leo hadi Jumapili.
Taarifa kutoka kwa idara hiyo inaarifu kuwa mafuriko hayo yanasababishwa na mvua kubwa inayotarajiwa nchini Ethopia na hivyo huenda maji yakafurika hadi katika maeneo hayo.
Wananchi katika kaunti hizo tatu wanashauriwa kuwa makini ili kuepuka hatari zinazosababishwa na mafuriko hayo.