Mwilu awaapisha wanachama wa jopo la kuwasaka makamishna wa IEBC

0

Kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu ameongoza hafla ya kuwaapisha watu saba watakaohudumu kwenye jopo la kuwatafuta makamishna wapya wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC).

Kwenye notisi iliyochapishwa Aprili 26, rais Uhuru Kenyatta aliwateua Elizabeth Muli, Gideon Solonka, James Awuori, Elizabeth Odundo, Dorothy Kimengech, Joseph Mutie na Farudin Abdalla kuhudumu kwenye jopo hilo.

Jopo hilo linatazamiwa kutoa mwaliko kwa umma kutuma maombi kujaza nafasi nne za makamishna wa tume hiyo ya IEBC chini ya siku saba baada ya kutangazwa wazi na rais.

Makamishna waliojiuzulu ni naibu mwenyekiti Consolata Nkatha, Roselyne Akombe, Margaret Mwachanya na Paul Kurgat.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here