Naibu Rais William Ruto amesema hatakubali kulazimishwa kuongoza kampeini za ‘LA’ kupinga marekebesho ya katiba kupitia mchakato wa BBI.
Akizungumza katika eneo bunge la Aldai, kaunti ya Nandi, Ruto amesema ataheshimu uamuzi utakaotolewa na Wakenya katika kura ya maamuzi na yuko tayari kuongoza taifa akitumia katiba ya zamani ama ile itabadilishwa kupitia BBI iwapo atachaguliwa kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.
Dr Ruto amedai kuwa wanaounga mkono BBI wamekuwa wakitumia vitisho kushinikiza wakenya kuunga mkono mabadiliko hayo ya katiba na badala yake anataka kila mkenya kuachwa kufanya uamuzi wake.









