Baba anayedaiwa kuwalipa watu kumuua mwanawe wa kiume eneo la Wendiga kaunti ya Nyeri atazuiliwa kwa muda wa siku tano zaidi.
Hakimu Mkuu wa mahakama ya Nyeri Mathias Okuche ameruhusu polisi waendelee kumzuilia Stephen Wangondu na washukiwa wenza watano ili kukamilisha uchunguzi kuhusu kesi hiyo.
Wangondu anatuhumiwa kuwalipa watu watano shilingi elfu mia moja sitini kumuua mwanawe Daniel Mwangi Januari mosi mwaka huu.
Washukiwa wengine ni James Mwangi, Geoffrey Waturi, Eddy Kariuki, Charity Muchiri na Raphael Wachira.
Wakaazi wa Mweiga waliandamana kushinikiza haki kwa marahemu.









