Shule kufunguliwa Jumatatu asema Magoha

0

Shule zitafunguliwa kwa muhula wa tatu Jumatatu ijayo chini ya masharti ya kuzuia msambao wa virusi vya corona.

Akizungumza alipofunga zoezi la kusahisha mtihani wa kidato cha nne KCSE, waziri wa elimu Profesa George Magoha amesema serikali imetuma pesa kwa shule mbalimbali ili kuhakikisha kuwa zimeajiandaa vilivyo kwa ufunguzi Jumatatu.

Hata hivyo amesema wanafunzi wa Gredi ya NNE watasalia nyumbani hadi Julai 26 wakati kalenda mpya ya masomo itakapoanza.

Profesa Magoha ameongeza serikali imetumia Sh7.5b kufadhili masomo katika shule za msingi na Sh2.8b kufadhili masomo katika shule za upili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here